Gossip

Bahati Ajitangaza Msanii Namba Moja Afrika Mashariki

Bahati Ajitangaza Msanii Namba Moja Afrika Mashariki

Staa wa muziki kutoka Kenya, Bahati, amejitangaza kuwa msanii namba moja nchini humo na Afrika Mashariki kwa ujumla baada ya wimbo wake wa kuomboleza kifo cha Raila Odinga kushika nafasi ya kwanza kwenye YouTube Trending Tab.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bahati amesema kuwa nyimbo zake mbili kushika nafasi ya kwanza na ya pili kwa wakati mmoja ni uthibitisho kuwa muziki wake unapendwa na Wakenya.

Msanii huyo amewataka wasanii wenzake wa Kenya kuchangamkia nafasi zilizobaki kwenye orodha ya nyimbo zinazotrend Youtube, ambazo kwa sasa nyingi zinashikiliwa na wasanii kutoka Tanzania.

Hata hivyo Bahati amesisitiza kuwa ataendelea kujiweka kileleni kwenye tasnia ya muziki nchini Kenya, akiwatahadharisha wasanii wenzake waliopanga kuachia nyimbo wiki ijayo kuahirisha mipango yao kwa kuwa naye pia anatarajia kuachia wimbo mwingine mpya ambao ni moto wa kuotea mbali

Wimbo wake “Bye Bye Baba”, ambao unamuenzi hayati Raila Odinga, umevutia zaidi ya milioni moja ya watazamaji ndani ya siku moja tangu uachiwe rasmi. Wakati huo huo, wimbo wake mwingine wenye utata “Seti” umevuka views milioni mbili ndani ya wiki mbili kwenye mtandao wa Youtube

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *