Entertainment

Familia ya Rapa Tory Lanez yamsameha Megan Thee Stallion

Familia ya Rapa Tory Lanez yamsameha Megan Thee Stallion

Familia ya rapa Tory Lanez imeweka wazi kumsamehe rapa Megan Thee Stallion. Baba mzazi wa rapa Tory Lanez, Sostar Peterson amethibitisha hilo kufuatia sakata la mwanae kukutwa na hatia ya makosa ya kumpiga risasi ya mguu rapa huyo Julai, mwaka 2020..

Kauli ya mzee huyo imekuja wiki chache baada ya kutoridhishwa na uamuzi wa Mahakama juu ya mwanae ambapo aliishtumu label ya Roc Nation ya Jay Z kuhusika katika uamuzi huo wa Mahakama.

Ikumbukwe, Tory Lanez alikutwa na hatia ya makosa yote matatu na kwa sasa yupo rumande akisubiri hukumu yake kusomwa Februari 28, mwaka 2023 akitazamia kifungo cha miaka 22 jela.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *