
Kuelekea fainali ya mchezo wa Kombe la Dunia Jumapili hii unaozikutanisha timu ya Taifa ya Argentina na Ufaransa, Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) limekataa ombi la Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kutaka kabla ya mchezo huo kuanza, ichezwe video yake uwanjani hapo ili kuhamasisha amani.
Imeelezwa kwamba Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliomba jambo hilo FIFA huku akitaka kuonekana katika video hiyo akitoa ujumbe wa kuhamasisha amani wakati huu Ukraine ikiwa katika vita kati yake na Urusi.
Taarifa za ndani kutoka vyanzo mbalimbali vya kuaminika zinaeleza kuwa, FIFA wamemkatalia Rais huyo wa Ukraine ombi hilo pasipo kumpa sababu za kukataa.