
Mchekeshaji maarufu nchini Kenya, Flaqo Raz, amekanusha madai ya kuwahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji na mrembo maarufu Trisha Khalid. Kupitia mahojiano aliyofanya hivi majuzi, Flaqo alieleza kwa uwazi kuwa madai hayo hayana ukweli wowote.
“It’s a lie, it never happened,” alisema Flaqo kwa msisitizo, akijibu uvumi uliokuwa ukienea mitandaoni kuhusu uwepo wa uhusiano wa kimapenzi kati yake na Trisha.
Kwa muda mrefu, mashabiki na watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakihusisha wawili hao, wakitumia picha na video walizowahi kufanya kazi pamoja kama ushahidi wa mapenzi kati yao. Hata hivyo, Flaqo amesema walikuwa tu marafiki wa kawaida waliokuwa wakishirikiana kwenye kazi na miradi ya kisanaa.
“Watu wana tabia ya kuchukulia kila interaction mtandaoni kama ishara ya uhusiano wa kimapenzi, lakini si kweli. Sijawahi toka na Trisha,” aliongeza.
Trisha Khalid bado hajajibu rasmi kuhusu kauli ya Flaqo, ingawa awali aliwahi pia kukanusha uvumi huo kupitia Insta Stories zake. Mashabiki wamepokea taarifa hii kwa hisia mseto, huku wengine wakisema walikuwa na matumaini kwamba wawili hao walikuwa wapenzi, kutokana na muonekano wa ukaribu wao.
Flaqo, ambaye pia ni muigizaji, mtayarishaji na msanii wa muziki, aliwataka mashabiki wake kuzingatia kazi na ubunifu wake badala ya maisha yake ya kibinafsi.