
Kama ulidhani mahusiano ya Stevo Simple Boy na Gee yalikuwa ya kweli ni kuambie tu pole, kwa sababu mrembo huyo amejitokeza hadharani na kukiri kuwa hajawahi toka kimapenzi na msanii huyo kama watu wengi wanavyochukulia mtandaoni.
Gee ambaye amekuwa akideka sana juu ya huba la Stevo Simple Boy kiasi cha kuwatishia wanawake kutomchumbia hitmaker huyo wa Wedding Day, amesema mahusiano yao yalikuwa ni kiki kwa ajili ya kuutangaza muziki wa Stevo Simple Boy.
Hata hivyo kauli ya mrembo huyo imeonekana kuwakera watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii ambao wametoa changamoto kwa wasanii kutoa muziki mzuri badala ya kuishi maisha ya kuigiza mtandaoni.
Utakumbuka mapema mwaka huu baada ya Stevo Simple Boy kumtambulisha Gee kama mpenzi wake na kumvisha pete ya uchumba alienda mbali zaidi na kuwaaminisha walimwengu kuwa wao ni mume na mke walipofanya harusi ya kitamaduni maarufu kama Ruracio kwa siri.