LifeStyle

Geoffrey Mosiria Amtolea Alicia Kanini Kazi Yenye Mshahara Mnono, Amshurutisha Kuacha Only Fans

Geoffrey Mosiria Amtolea Alicia Kanini Kazi Yenye Mshahara Mnono, Amshurutisha Kuacha Only Fans

Mwanaharakati na mhamasishaji wa maadili ya jamii, Geoffrey Mosiria, ametoa ofa ya kazi kwa mjasiriamali wa kidijitali na content creator, Alicia Kanini, yenye mshahara wa kati ya KSh 50,000 hadi KSh 100,000 kwa mwezi  lakini kwa masharti makali.

Kwenye mahojiano maalum, Mosiria alisema yuko tayari kumsaidia Alicia kujikwamua kimaisha kupitia kazi halali, lakini ni lazima aachane na shughuli zake za OnlyFans (OF), jukwaa maarufu kwa maudhui ya watu wazima ambalo Alicia amekuwa akilitumia kujipatia riziki.

 “Alicia Kanini ni mdada mrembo na mchapa kazi. Niko tayari kumpa kazi inayolipa vizuri, mshahara kati ya elfu hamsini hadi laki moja, lakini ni lazima aache maisha ya OF. Tunataka kumuinua kwa njia ya heshima,” alisema Mosiria kwenye mahojiano na 2mbili.

Kauli hiyo imepokelewa kwa hisia mseto, huku baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wakimsifu Mosiria kwa kuonyesha mfano wa kuunga mkono vijana kwa njia ya heshima, ilhali wengine waliona kama ni jaribio la kumdhibiti Alicia au kumdhalilisha kwa njia ya hadharani.

Alicia, ambaye ni maarufu kwa maudhui yake ya kuvutia maelfu ya wafuasi, bado hajatoa majibu rasmi kuhusiana na ofa hiyo. Hata hivyo, mashabiki wake wamejitokeza kwa wingi wakimtaka aendelee na kile anachoamini, huku wengine wakihimiza akubali nafasi hiyo kama hatua ya kuanza maisha mapya.