Mrembo maarufu mtandaoni nchini Kenya Gloria Ntazola, anayejulikana kama Kanjo Lady, ameweka wazi kuwa hana mpango wa kufanyiwa upasuaji wa kuongeza makalio (Brazilian Butt Lift) licha ya mashinikizo kutoka kwa baadhi ya wafuasi wake mitandaoni.
Gloria, ambaye hivi karibuni amefichua kuwa alifanyiwa upasuaji wa kuongeza maziwa na kuminya kiuno nchini Nigeria, amesema kuwa watu wengi wamekuwa wakimshawishi afanye BBL ili kukamilisha umbo lake.
Kwa mujibu wa maelezo yake, makalio yake ya asili tayari ni makubwa, na haoni sababu ya kuongeza au kubadilisha chochote katika eneo hilo. Mrembo huyo amesema anaamini katika kufanya marekebisho anayoona yanafaa kwake binafsi, lakini si kufuata presha ya mitandaoni.
Kauli yake imezua mjadala mitandaoni, baadhi ya watu wakimuunga mkono kwa kusimama na maamuzi yake ya urembo, huku wengine wakiendelea kutoa maoni tofauti kuhusu mabadiliko ya mwili kwa njia ya upasuaji.