Entertainment

VJ Patelo Awakosoa Arrow Bwoy na Masauti Kwa Wimbo Wao Mpya ‘Kilimani’

VJ Patelo Awakosoa Arrow Bwoy na Masauti Kwa Wimbo Wao Mpya ‘Kilimani’

Mwanamitandao maarufu nchini Kenya, VJ Patelo, ameibua gumzo baada ya kutoa kauli kali dhidi ya wimbo mpya wa Arrow Bwoy na Masauti unaoitwa Kilimani.

Kupitia mitandao ya kijamii, Patelo amekosoa vikali kazi hiyo akidai haina ubora na kwamba haitapata mashiko kwenye tasnia ya muziki. Amesema kuwa wimbo huo utabaki kusikilizwa na wasanii hao wenyewe pekee, akiwashutumu kwa kile alichokitaja kama kuleta mzaha katika muziki wa Kenya.

Katika malalamiko yake, Patelo amewashutumu wasanii hao akisema kuwa tasnia haihitaji wasanii wanaotoa kazi ambazo hazina ubunifu au ubora wa kuvutia.

Aidha, amemkebehi Arrow Bwoy kwa kumlinganisha na jina la mitaani “Arrow Roots,” akionyesha kutoridhishwa kabisa na kazi waliyoitoa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *