Tech news

Google Yaleta “AI Mode” Katika Search Engine Yake

Google Yaleta “AI Mode” Katika Search Engine Yake

Google imezindua mfumo mpya wa “AI Mode” katika injini yake ya utafutaji, unaowezesha watumiaji kuchat moja kwa moja na Google Search kama wanavyofanya na ChatGPT. Hii inalenga kuboresha uzoefu wa utafutaji kwa kutumia teknolojia ya akili bandia.

Kampuni hiyo pia imeongeza mfumo wa kisasa wa AI uitwao Gemini 2.5, ambao una uwezo mkubwa wa kuelewa na kuchakata lugha, hivyo kusaidia kutoa majibu sahihi na ya haraka zaidi kwa watumiaji.

Mabadiliko haya ni sehemu ya juhudi za Google kuimarisha huduma zake za utafutaji kwa kutumia AI, huku ikilenga kushindana na majukwaa mengine ya teknolojia kama OpenAI na Microsoft. Mfumo huu mpya unatarajiwa kuanza kupatikana kwa awamu duniani kote.

Watumiaji wataweza kutumia AI Mode kusaidia katika shughuli mbalimbali kama kutafuta bidhaa, kupanga ratiba, au kutafuta taarifa kwa haraka zaidi, na hivyo kubadilisha jinsi watu wanavyotumia mtandao katika maisha ya kila siku.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *