Entertainment

Gravity Omutujju Amaliza Urafiki na King Saha kwa Uchungu Mwingi

Gravity Omutujju Amaliza Urafiki na King Saha kwa Uchungu Mwingi

Msanii wa muziki wa hip-hop nchini Uganda, Gravity Omutujju, amezungumza kwa mara ya kwanza kwa kina kuhusu kuvunjika kwa urafiki wake na mwanamuziki King Saha, akifichua kuwa hana tena uhusiano wowote naye.

Wawili hao walikuwa marafiki wa karibu kwa muda mrefu na walishirikiana katika kibao kilichopata umaarufu kiitwacho “Winner”. Hata hivyo, uhusiano wao uliingia doa mwezi Septemba mwaka jana baada ya King Saha kusherehekea hadharani kufeli kwa tamasha la Gravity, kitendo kilichomvunja moyo na kumwacha na maumivu makali.

Akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni, Gravity alisema wazi kuwa hana nia ya kurejesha urafiki huo, licha ya kutokuwa na chuki ya moja kwa moja.

β€œSina ugomvi naye, lakini si rafiki yangu tena. Sitaki kuwa na uhusiano wowote naye. Tulikuwa marafiki wa dhati, lakini niliumia sana kwa alichokifanya. Siwezi kumsamehe, wala kusahau,” alieleza kwa hisia.

Kauli hiyo imezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii, ambapo mashabiki wameonyesha hisia mseto, wengine wakisikitishwa na kuvunjika kwa urafiki huo, huku baadhi wakimuunga mkono Gravity kwa msimamo wake.

Ingawa haijulikani iwapo wawili hao wataweza kusameheana na kurejesha urafiki wao wa zamani, kwa sasa, dalili zote zinaonyesha kuwa mlango huo umefungwa kabisa.