Msanii wa muziki wa Injili, Guardian Angel, ametoa onyo kali kwa watumiaji wa mitandao wanaoeneza chuki na kuwakandamiza wengine kupitia maneno ya kashfa na matusi.
Kupitia ujumbe wake mtandaoni, Guardian Angel amesema kuwa watu wengi wanaumizwa na maudhui ya chuki yanayoenezwa bila kujali hisia zao, akibainisha kuwa wengi wao hupitia mateso makubwa kimya kimya kutokana na maneno ya ukatili yanayorushwa dhidi yao bila huruma.
Amesisitiza kuwa wale wanaotumia mitandao kuumiza wengine kwa lugha za kudhalilisha watawajibika siku moja, akisema hakuna atakayeweza kutoroka matokeo ya matendo yake.
Guardian Angel amewataka watumiaji wa mitandao kutumia majukwaa yao kwa ajili ya kujenga na kuhamasisha upendo, badala ya kutumika kama chanzo cha chuki, majeraha ya kiakili na machafuko ya kijamii.