Msanii mkongwe kwenye gemu ya Bongo Fleva, 20 Percent, ametoa kauli nzito kuhusu wimbi la wasanii kutoa nyimbo zenye matusi, akisema suluhisho si kufungia kazi hizo bali kuwaadhibu moja kwa moja wasanii wanaohusika.
Akizungumza kupitia kipindi cha Funky Friday, 20 Percent amesema kuwa hatua ya mamlaka husika kufungia au kuzuia nyimbo haitoshi kudhibiti maudhui machafu, akisisitiza kuwa adhabu kali dhidi ya wasanii ndio itakayowazuia kurudia makosa.
Amesema wazi kuwa, ili kulinda maadili ya jamii na kizazi kinachokua, ni muhimu kuangalia chanzo hasa wasanii wanaotunga na kurekodi matusi badala ya kupambana na matokeo pekee.
Kwa mujibu wa 20 Percent, kufungwa jela kwa wasanii wanaoimba matusi kutakuwa fundisho na onyo kwa wengine wanaofikiria kuchafua taswira ya muziki wa Bongo Fleva kwa maudhui yasiyofaa.