Mrembo na mfanyabiashara kutoka Tanzania, Hamisa Mobetto, amefunguka baada ya tetesi za ujauzito wake kusambaa kwa kasi mtandaoni.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Stories, Hamisa ameamua kuvunja ukimya na kuweka wazi msimamo wake kuhusu habari hizo ambazo zimezua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki na wadau wa mitandao ya kijamii.
Hamisa amesema kuwa kama kweli kuna mtu tayari amesambaza taarifa hizo, basi haoni tatizo kwani yeye yuko huru kabisa kuwa mjamzito. Ameeleza kuwa ujauzito si kosa wala jambo la kumuumiza mtu yeyote, na iwapo taarifa hizo ni za kweli, basi ni jambo la furaha kwake kuzaa na mume wake Aziz Ki.
Hata hivyo, Hamisa hakuthibitisha moja kwa moja iwapo kweli ni mjamzito, lakini ujumbe wake umeonesha wazi kuwa yuko katika hali ya amani na furaha kuhusu maisha yake ya sasa.