Gossip

Huddah Monroe Atangaza 2025 Kuwa Mwisho wa Kuvumilia Waliomkosea

Huddah Monroe Atangaza 2025 Kuwa Mwisho wa Kuvumilia Waliomkosea

Socialite kutoka nchini Kenya, Huddah Monroe, ametuma ujumbe mzito unaoashiria mabadiliko makubwa katika maisha yake binafsi, akisema kuwa mwaka 2025 ndio mwisho wa kuvumilia watu waliomkosea.

Kupitia ukurasa wake wa Insta Story, Huddah ameweka wazi kuwa amechoka kutoa nafasi ya pili kwa watu wanaomuumiza au kuvunja imani yake. Ameeleza kuwa kuanzia mwaka 2026, hatakuwa tayari kusamehe tena makosa, iwe ni kutoka kwa marafiki wa karibu au hata wanafamilia.

Kwa mujibu Huddah, mwaka 2025 ulikuwa mwaka wa mwisho kwake kuwapa watu nafasi ya pili, akisisitiza kuwa yeyote atakayemvunjia heshima hata kama ni mtu wa familia, atamuondoa kabisa katika maisha yake bila kumpa nafasi nyingine.

Kauli hiyo imezua mjadala mkubwa mitandaoni, ambapo baadhi ya mashabiki wake wameonyesha kumuunga mkono wakisema ni muhimu kulinda amani ya nafsi, huku wengine wakiona msimamo huo kuwa mkali hasa inapohusisha familia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *