Staa wa mitindo na muziki kutoka Tanzania, Hamisa Mobetto, amepewa zawadi ya gari jipya la kifahari aina ya Mercedes-Benz G-Class (G-Wagon) na mumewe Stephane Aziz Ki, ikiwa ni zawadi ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu wafunge ndoa.
Kupitia picha na video zilizosambaa mitandaoni, Hamisa ameonekana mwenye furaha akipokea zawadi hiyo ya thamani kubwa, huku akimshukuru mumewe kwa upendo na heshima anayoendelea kumuonesha.
Gari aina ya G-Wagon linatajwa kuwa miongoni mwa magari ya kifahari na ghali zaidi duniani, jambo lililofanya mashabiki wengi kuwapongeza kwa hatua hiyo ya kimahaba.
Mashabiki wengi wamewapongeza kwa kuendelea kuonesha mfano wa ndoa yenye upendo na kuheshimiana, huku wengine wakieleza kuwa zawadi hiyo ni uthibitisho wa thamani na nafasi ya kipekee aliyonayo Hamisa katika maisha ya mchezaji huyo kutoka Burkina Faso.