
Msanii wa muziki kutoka 001 music Happy C ametangaza ujio wa EP yake mpya ambayo ana mpango wa kuachia ndani ya mwaka huu wa 2022.
Akiwa kwenye moja ya interview happy C amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kuipokea EP yake hiyo ambayo kwa mujibu wake itakuwa na jumla ya mikwaju 5 ya moto.
Hata hivyo hajeweka wazi jina la EP wala tarehe rasmi ambayo EP yenyewe itaingia sokoni ila amesema uongozi wake wa 001 music ndio utahamua siku ambayo EP yake hiyo itaachiwa.
Hii unaenda kuwa EP ya pili kwa mtu mzima Happy C ikizingatiwa kuwa mwaka wa 2021 aliwabariki mashabiki zake na EP iitwayo Karata tatu ambayo ilikuwa na jumla ya mikwaju tatu ya moto.