
Msanii kutoka 001 music Happy C ameoneshwa kusikitishwa na kitendo cha Akeelah kutangaza kuacha muziki.
Kwenye mahojiano na Captain Nyota amesema Akeelah ni msanii mwenye kipaji cha kipekee kwenye muziki wa Kenya, hivyo hapaswi kukata tamaa kwenye harakati za kuipambania ndoto yake kwa kuwa muziki una changamoto nyingi.
Happy C amemshauri kujifikiria tena kutokana na maamuzi magumu ambayo ameyachukua kwenye muziki wake na atumie changamoto kama kigezo cha kufanya makubwa.
Kauli yake imekuja baada ya Akeelah kusema ameamua kuacha muziki kwa sababu ya maonevu na unyanyasaji alioupitia katika safari yake ya mziki.
Hitmaker huyo wa Tujikumbushe, alienda mbali Zaidi na kuushukuru uongozi wa Hakim Empire kwa mchango wao kwake huku akikosa kuutaja uongozi wa Shirko Media ambao ulimlea kimziki.