Sports news

Harambee Stars Yacharazwa 8–0 na Senegal Uturuki

Harambee Stars Yacharazwa 8–0 na Senegal Uturuki

Timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, imepata matokeo mabaya zaidi katika historia ya mechi zake za kirafiki baada ya kulala 8–0 dhidi ya miamba wa Afrika Senegal, kwenye mchezo uliopigwa jana usiku nchini Uturuki.

Mchezaji nyota wa Al-Nassr na zamani wa Liverpool, Sadio Mane, aling’ara kwa kufunga hat-trick, huku mshambulizi wa Bayern Munich Nicolas Jackson akiongeza mabao mawili. Mabao mengine yalifungwa na Malik Diouf wa West Ham United, Ibrahim Mbaye wa PSG, pamoja na Cherif Ndiaye wa Samsunspor.

Huu unakuwa mchezo wa pili mfululizo Harambee Stars kupoteza ndani ya siku nne, baada ya kukubali kichapo cha 1–0 dhidi ya Equatorial Guinea katika mechi nyingine ya kirafiki.

Kwa upande wa Senegal, ushindi huu ulikuwa dawa ya kurejesha morali baada ya kukosa kufunga dhidi ya Brazil katika mchezo wao uliopita ambao walishindwa mabao 2–0.

Stars wanacheza mechi zenye ushindani mkubwa kama sehemu ya maandalizi kuelekea fainali za AFCON 2027, ambazo zitafanyika kwa mara ya kwanza katika Afrika Mashariki, zikiandaliwa kwa ushirikiano na Kenya, Uganda na Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *