Gossip

Harmonize Aibua Maswali kwa Kuficha Sura ya Mpenzi Mpya

Harmonize Aibua Maswali kwa Kuficha Sura ya Mpenzi Mpya

Msanii nyota wa Bongo Fleva, Harmonize, ameibua gumzo mitandaoni baada ya kuonyesha dalili za kuwa kwenye uhusiano mpya wa kimapenzi.

Kupitia Insta Story yake, Harmonize amepost picha na video zikimuonesha akiwa na mrembo anayesemekana kuwa mpenzi wake mpya huku akificha sura yake. Hatua hiyo imezua minong’ono miongoni mwa mashabiki ambao wamekuwa wakijiuliza ni nani haswa mpenzi huyo mpya wa mkali huyo wa Best Couple.

Tetesi hizo zimezidi kushika kasi baada ya video nyingine kusambaa, ikimuonesha Harmonize akiwa amelala pembezoni mwa mrembo huyo. Tukio hilo limeibua mjadala kuhusu ni kwa nini staa huyo anaamua kuficha sura ya mchumba wake mpya ilhali tayari kumekuwepo na ushahidi wa video kuvuja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *