Entertainment

Harmonize akanusha kumdai Anjella shillingi millioni 52

Harmonize akanusha kumdai Anjella shillingi millioni 52

Bosi wa lebo ya Konde Music Worldwide, Msanii Harmonize ameamua kuvunja kimya chake juu ya stori zinazotembea mtandaoni kuhusu kumkimbia msanii wake Anjella.

Kupitia instastoy yake Harmonize ameweka wazi kuwa ni kweli amefika mwisho wa kumsapoti Anjella, hivyo kwa yeyote mwenye uwezo anaruhusiwa kumshika mkono msanii huyo bila pingamizi.

Hitmaker huyo wa “Leave Me Alone amesema kuwa hamdai pesa yoyote Anjella kama malipo ya kuachana na lebo ya Konde Gang huku akiwataka watu kupuuza mambo ya uongo yanayoendelea mtandaoni.

“Nilikutana na Anjella akiwa amejikatia tamaa akiwa na ndoto kichwani, sikujiangalia nina kiasi gani niliamini kuwa wapo wanaonisapoti bila kuwalipa senti 5 basi watasapoti kipaji cha sister Anjella”.

“Nilichoangalia ni ndoto hasa za mtoto wa kike nimejitahidi kadri ya uwezo wangu najua kuna wenye uwezo mkubwa kunizidi ukizingangatia nimeanza juzi”

“Kama kuna anayeweza kumuendeleza kipaji chake ni faraja kwangu asisite kujitokeza. Puuzia siasa za kusema sijui namdai mahela sikumuuliza kuhusu pesa hata senti 1”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *