Entertainment

HARMONIZE AMTAKA ALI KIBA KUTUMBUIZA KATIKA SIKU YAKE YA UCHUMBA

HARMONIZE AMTAKA ALI KIBA KUTUMBUIZA KATIKA SIKU YAKE YA UCHUMBA

Mwanamuziki Maarufu nchini Tanzania, Harmonize ameonesha heshima kwa mwanamuziki mwenzake Alikiba kwa kumpongeza kwa kazi nzuri anayofanya kwenye tasnia ya Muziki wa Bongofleva.

Kupitia ukurasa wake wa instagram, Harmonize alichapisha video fupi iliyokuwa ikicheza wimbo mpya wa Alikiba unaoitwa ‘Utu’ huku akiambatinisha na ujumbe kwamba siku ya kuvisha pete mpenzi wake lazima King Kiba atumbuize mashabiki wake.

“Mtu amwambie mkongwe, mfalme Ali Kiba lazima aimbe kwenye usiku wa kumvisha pete mchumba wangu, huu muziki mzuri sana,” Harmonize aliandika.

Utakumbuka juzi kati wanamuziki hao walionekana wakisafiri kwenye ndege pamoja jambo ambalo liliteka mazungumzo mtandaoni kwa muda

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *