Gossip

Harmonize na Kajala Washindwa Kujizuia Jukwaani, Wapigana Mabusu Hadharani

Harmonize na Kajala Washindwa Kujizuia Jukwaani, Wapigana Mabusu Hadharani

Msanii wa Bongo Fleva Harmonize na Mwanamama Kajala Masanja wamezua gumzo kubwa baada ya kuonekana wakishindwa kujizuia jukwaani na kupigana mabusu hadharani, tukio lililotokea usiku wa kuamkia leo wakati wa burudani huko Visiwani Zanzibar.

Wakiwa mbele ya maelfu ya mashabiki, wawili hao walionekana wakitabasamu, kukumbatiana na hatimaye kubadilishana mabusu, jambo lililosababisha shangwe na makelele kutoka kwa mashabiki waliokuwepo.

Kitendo hicho cha kupigana mabusu jukwaani kimezua tafsiri tofauti, huku baadhi ya mashabiki wakiamini ni ishara ya kurudiana rasmi, na wengine wakidai huenda ilikuwa ni sehemu ya burudani.

Video na picha za tukio hilo zimesambaa kwa kasi mitandaoni, zikifanya jina la Harmonize na Kajala kutrendi. Bila shaka, tukio hili limeongeza ukurasa mpya katika simulizi la mahusiano ya Harmonize na Kajala, simulizi linaloendelea kuvuta hisia za wengi ndani na nje ya tasnia ya burudani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *