
Msanii wa Bongofleva, Rayvanny ametapika nyongo kumuhusu Harmonize, ni vita ya maneno ambayo ilianzia kwenye insta story kufuatia Harmonize kuwataka wasanii kuacha kuimba nyimbo za kutukuza pombe kwani zinaharibu Jamii.
Tamko hili lilimgusa Rayvanny ambaye aliibuka na kumjibu Harmonize kwamba, asiongee chochote kuhusu nyimbo za pombe kwani hajawahi kufanya nyimbo za aina hiyo na zikafanya vizuri. Rayvanny hakuishia hapo, ni kama alikuwa amekaa na kitu rohoni kwa muda mrefu sana kuhusu Harmonize.
Kupitia insta story yake usiku wa kuamkia leo ameongea mengi ikiwemo kumchana Harmonize kuwa ana roho mbaya, mbinafsi kwa kutaka kumfunga Jela kufuatia lile sakata la mtoto wa Kajala, Paula.
Mmiliki huyo wa Next Level Music, aliendelea kutema nyongo kwa kusema amemsaidia Harmonize kimuziki ikiwemo kumuandikia verse nzima kwenye wimbo wa “Paranawe” na “Happy Birthday” lakini pia alifunguka kwamba, ameilipa lebo ya WCB shillingi milioni 53 za Kenya lakini hakuwahi kufungua mdomo wake kuongea.