LifeStyle

Huddah Monroe Afunguka Namna Marehemu Silas Jirongo Alivyombadilisha Maisha Yake

Huddah Monroe Afunguka Namna Marehemu Silas Jirongo Alivyombadilisha Maisha Yake

Socialite kutoka Kenya Huddah Monroe amefunguka kwa hisia kali kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge nchini humo, marehemu Cyrus Jirongo, akieleza namna alivyomsaidia kifedha kwa kiasi kikubwa na kumtoa kwenye hali ngumu ya maisha.

Kupitia ujumbe wake wa rambirambi aliouchapisha mitandaoni, Huddah amesema msaada wa Jirongo ulikuwa wa kipekee na wa kubadilisha maisha, akisisitiza kuwa ni mmoja wa watu wachache waliomsaidia bila masharti.

Katika ujumbe huo, Huddah amesema kuwa mara nyingi kumekuwepo na dhana kwamba watu wa jamii ya Waluhya hawatoi pesa, lakini kwa upande wake Jirongo alimthibitishia kinyume chake kwa vitendo.

Huddah amesema msaada alioupata kutoka kwa Jirongo ulimtoa kabisa kwenye lindi la umaskini, hatua ambayo ilimfungulia ukurasa mpya wa maisha na mafanikio aliyofikia leo.

Kifo cha Cyrus Jirongo kimetokea mapema jana baada ya kuhusika katika ajali mbaya ya barabarani kwenye barabara kuu ya Nakuru–Nairobi, tukio lililoshtua taifa la Kenya na kuacha majonzi makubwa kwa familia, marafiki na watu waliowahi kuguswa na ukarimu wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *