Gossip

Huddah Monroe Azua Tetesi za Mahusiano na Rapa Rick Ross

Huddah Monroe Azua Tetesi za Mahusiano na  Rapa Rick Ross

Rapper wa Marekani Rick Ross ameibua gumzo jipya la tetesi za kimapenzi na sosholaiti wa Kenya Huddah Monroe baada ya kutuma ujumbe wa faragha uliodhihirisha ukaribu wao.

Huddah, kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameshare screenshot ya mazungumzo yao na kuandika ujumbe ulioashiria kujisalimisha kwake kwa mapenzi ya msanii huyo. Katika maelezo yake, Huddah amesisitiza kuwa yuko tayari kumfuata Rick Ross kwa chochote anachotaka, akimtaja kuwa ndiye mwenye mamlaka na uongozi katika mawasiliano yao.

Maneno aliyoyaweka yalionesha wazi namna anavyomuona msanii huyo kama mtu muhimu kwake na namna anavyompa kipaumbele katika maisha yake ya kimtandao. Hatua hiyo imewafanya wengi kuamini kuwa wawili hao huenda wako katika hatua za mwanzo za uhusiano.

Mashabiki mitandaoni wamekuwa na maoni mseto, baadhi wakisema wawili hao wamekuwa na ukaribu kwa muda mrefu, huku wengine wakidai huenda ni maandalizi ya promo au mradi mpya utakaowahusisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *