Msanii Iyanii, ameahidi kuwatunuku wachezaji wa timu ya taifa ya Harambee Stars kwa kuandaa tamasha bure maalum, ikiwa ni njia yake ya kuwapongeza kwa uchezaji wao bora kwenye michuano ya CHAN 2024.
Kupitia Ukurasa wake Instagram ameshindwa kuficha furaha yake kwa mafanikio ya timu hiyo na kupongeza kitendo cha wachezaji kumuonyesha upendo mkubwa kupitia hit single yake iitwayo Donjo Maber ambayo kwa mujibu wake ni moja kati ya ngoma pendwa zaidi kwa wachezaji wa timu ya taifa.
Kauli ya Iyanii inakuja wakati ambapo Harambee Stars imekuwa ikionyesha matokeo mazuri katika mashindano hayo, hasa baada ya timu hiyo kupokea zawadi ya mamilioni ya fedha kutoka kwa Rais William Ruto kama motisha kwa mafanikio yao.
Tamasha hilo linalopangwa litakuwa ishara ya kusherehekea juhudi na kujitolea kwa wachezaji wa Stars, huku pia likionekana kama hatua ya kuunganisha mashabiki wa soka na muziki nchini.
Iwapo mipango itakamilika, hafla hiyo inatarajiwa kuwa moja ya matukio makubwa ya burudani mwaka huu, mashabiki wakisubiri kutangaziwa tarehe na mahali ambapo tamasha hilo litafanyika