
Rapa kutoka nchini Marekani J. Cole amefunguka na kusema kwamba yeye ndiye alimuweka Kendrick Lamar kwenye ramani ya muziki wa Hiphop.
Kwenye mahojiano na mtangazaji Nardwuar, Cole amekiri kuwa yeye ndiye alimshawishi Dr. Dre amsaini Kendrick kwenye lebo ya muziki ya Interscope Records pamoja na Aftermath Entertainment mwaka wa 2012.
Baada ya kuulizwa swali hilo na Nardwuar , J. Cole alisita kwa sekunde 15 na kushangaa kidogo kisha akasema“Ni nani amekwambia kuhusu hili? Ni nani amekupa hii taarifa? Jibu ni ndio. Nilifanya hivyo. Siwezi kusema mimi ndio nilikuwa wa kwanza kumwambia, nilipomfikisha kwa Dre nilimwambia [Dre] unajua cha kufanya. Nampongeza Dre kwa uchaguzi sahihi.”
Ikumbukwe Mwezi Machi mwaka 2012 Kendrick Lamar alisainiwa rasmi na Interscope Records pamoja na Aftermath Entertainment hivyo kuhitimisha safari yake ya kuwa msanii wa kujitegemea. Kazi yake ya kwanza chini ya label hiyo ilikuwa ni (good kid, m.A.A.d city) ambayo ni album yake ya pili.