Entertainment

Jose Chameleone aeleza sababu za kumuunga mkono Rais Museveni

Jose Chameleone aeleza sababu za kumuunga mkono Rais Museveni

Mwanamuziki nguli kutoka Uganda, Jose Chameleone, ameeleza sababu zinazomfanya aendelee kumuunga mkono Rais Yoweri Museveni na chama tawala cha NRM, licha ya ukosoaji kutoka kwa baadhi ya wananchi.

Akizungumza kwenye mahojiano maalum, Chameleone amesema uhusiano wake na Rais Museveni unatokana na heshima, shukrani, na imani kwamba chama hicho ndicho kimekuwa sehemu ya maisha yake tangu utotoni.

Ameeleza kuwa anamheshimu Rais Museveni kama kiongozi mwenye uvumilivu, anayefanya maamuzi kwa busara na asiyeongozwa na hisia.

Mwanamuziki huyo pia amefichua kuwa Rais Museveni aliwahi kumsaidia kifedha wakati alipokuwa akisumbuliwa na maradhi akiwa nchini Marekani, jambo analolitaja kama ishara ya utu na uongozi bora.

Chameleone amesema ataendelea kuwa mwaminifu kwa Rais Museveni na chama cha NRM, akisisitiza kuwa anaamini kiongozi huyo ameendelea kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya taifa la Uganda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *