Entertainment

Jose Chameleone Akataa Kukabidhi Mali Zake kwa Daniella Kabla ya Kifo

Jose Chameleone Akataa Kukabidhi Mali Zake kwa Daniella Kabla ya Kifo

Mwanamuziki nguli wa Uganda, Jose Chameleone, ameibua mjadala baada ya kuweka wazi kuwa hatakubali kukabidhi mali zake akiwa bado hai, licha ya mkewe Daniella kutaka usimamizi wa baadhi ya mali hizo katika shauri la talaka linaloendelea.

Chameleone amesema mali alizojipatia ni kwa ajili ya watoto wake na anataka warithi mali hizo baada ya kifo chake, ili nao wazikabidhi kwa wajukuu wake. Hata hivyo, amesisitiza kuwa hatalazimishwa kuandika wasia mapema kwani anaamini bado ni jukumu lake kulinda urithi huo akiwa hai.

Amefafanua kuwa shauri la talaka linaloendelea ni sawa na kumtaka aandike wasia kabla ya kifo chake, jambo analoliona halina mashiko. Pia amekanusha taarifa kwamba anaishi na msongo wa mawazo, akibainisha kuwa anaendelea vizuri na ana mtazamo wa kutambua kuwa mali ni vitu vya kupita ambavyo havipaswi kusababisha wasiwasi.

Chameleone ameongeza kuwa, licha ya tofauti zilizopo kati yake na Daniella, wote wawili wanapigania lengo moja, kuhakikisha watoto wao wanapata maisha bora na urithi wa familia unabaki mikononi mwao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *