Entertainment

Juma Jux Ampongeza Diamond kwa Kufungua Milango ya Kimataifa kwa Wasanii wa Bongo

Juma Jux Ampongeza Diamond kwa Kufungua Milango ya Kimataifa kwa Wasanii wa Bongo

Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Juma Jux, amempongeza Diamond Platnumz kwa mchango wake mkubwa katika kufungua njia za kimataifa kwa wasanii wa Tanzania.

Akizungumza katika mahojiano na El Mando TZ, Jux amesema kuwa Diamond ameonyesha mfano wa kuigwa kupitia matamasha yake makubwa aliyoandaa nchini Uingereza, ikiwemo London, Manchester na Glasgow mwezi Julai, ambayo yalitoa fursa kwa muziki wa Tanzania kufika hadhira ya kimataifa.

Jux amesisitiza kuwa hatua kama hizo ni muhimu katika kuinua tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, hasa pale msanii mmoja anapowapa nafasi wenzao kupata exposure kupitia majukwaa ya kimataifa.

Jux ametolea mfano wasanii wa Nigeria ambao wanapoenda kufanya maonesho barani Ulaya, kama vile katika ukumbi wa O2 Arena, huwa hawasahau kuwashirikisha wasanii wenzao wa nyumbani.

Hata hivyo amesema kuwa ni muhimu kwa wasanii wa Tanzania pia kuendeleza utamaduni huo wa kusaidiana, ili kuhakikisha muziki wa Bongo Fleva unaendelea kupanuka na kushindana kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *