Muigizaji wa Bongo Movie Kajala Masanja amefunguka kuwa mwanamuziki Harmonize ambaye kwa sasa ni mume wake aliwahi kumlipia binti yake Paula Kajala ada ya shule alipokuwa akisoma kidato cha pili (Form Two).
Kwa mujibu wa Kajala, msaada huo ulikuja katika wakati muhimu wa masomo ya Paulah, jambo analosema linadhihirisha namna Harmonize alivyokuwa tayari kubeba majukumu hata kabla ya mahusiano yao kuwa wazi kwa umma.
Mwanamama huyo, amesema uhusiano wao haukuwa wa muda mfupi kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakidhani, bali ulianza zamani na ulihusisha pia majukumu ya kifamilia.
Hata hivyo, Kajala amesisitiza kuwa aliamua kusema hayo ili kuweka wazi ukweli wa maisha yake binafsi, akibainisha kuwa mengi yalibaki siri kwa muda kabla ya kuwekwa wazi kwa umma.