Gossip

Q Chief Azua Gumzo Baada ya Kutishia Kumpiga Mtangazaji wa EATV

Q Chief Azua Gumzo Baada ya Kutishia Kumpiga Mtangazaji wa EATV

Msanii mkongwe wa Bongofleva, Q Chief amezua gumzo mitandaoni baada ya kutishia kumtwanga mtangazaji wa EATV, kufuatia madai yaliyoibuliwa wakati wa mahojiano kuwa ana mpango wa kuacha muziki kutokana na malipo duni ya shoo.

Kwa mujibu wa video zinazotembea mtandaoni, msanii huyo ameonekana kuchukulia mada hiyo kama ya kumkera na kumdhalilisha, akisisitiza kuwa suala la kuacha muziki ni nyeti na halipaswi kuzungumzwa kwa namna ya kubeza juhudi zake.

Tukio hilo linadaiwa kutokea alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha burudani cha EATV, ambapo mtangazaji alimuuliza kuhusu taarifa zinazosambaa kwamba amechoshwa na tasnia ya muziki kwa sababu ya kulipwa kiasi kidogo licha ya kufanya kazi kubwa jukwaani. Swali hilo halikumkaa sawa Q Chief, hali iliyomfanya kuonyesha hasira na kutoa kauli kali iliyotafsiriwa kama tishio

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *