
Kaka wa rapa Young Thug aitwaye Quantavious Grier “Unfoonk” amekiri makosa yake mahakamani na kuingia makubaliano maalumu kwamba asiwe na mawasiliano na Young Thug.
Kwa mujibu wa Wbstv rekodi za mahakama ya jimbo la fulton zinaonyesha kuwa Quantavious Grier alikiri shtaka moja la kukiuka sheria inayopambana na rushwa (rico) na shtaka moja la wizi kwa kupokea mali ya wizi.
Unfoonk, alikubali kifungo cha miaka 12 huku miaka miwili ikibadilishwa kuwa muda uliotumika na miaka 10 ni kifungo cha nje chini ya uangalizi
Hata hivyo kuna masharti ambayo Grier atalazimika kuyatimiza kama sehemu ya kifungo chake cha nje.
Masharti hayo ni pamoja na asifanye mawasiliano yoyote na kaka yake Young Thug pamoja na washtakiwa wengine hadi kesi hiyo imalizike.
Lakini pia katika saa 750 afanye shughuli za kijamii lakini kutotoka nje na kutomiliki bunduki.