Entertainment

KANYE WEST AMTAKA BILLIE EILISH KUMUOMBA MSAMAHA TRAVIS SCOTT KWA KUMVUNJIA HESHIMA

KANYE WEST AMTAKA BILLIE EILISH KUMUOMBA MSAMAHA TRAVIS SCOTT KWA KUMVUNJIA HESHIMA

Rapa Kanye West ameonesha mahaba kwa rafiki yake wa karibu kabisa Travis Scott, kwani ametishia ujiondoa kwenye tamasha la Coachella mpaka pale mwanamuziki mwenzake Billie Eilish atakapomuomba msamaha travis scott kwa kum-diss kwenye moja ya tamasha lake alilofanya wikendi iliyopita.

Billie Eilish alim-diss Travis Scott kwenye tamasha lake akidai kuwa yeye huwa anasitisha show kama mashabiki wakiwa katika hali mbaya.

Kauli ambayo ilitajwa kumlenga rapper Travis Scott ambaye aliripotiwa kushindwa kusitisha tamasha lake la Astro-World festival baada ya baadhi ya mashabiki kufariki na wengine kujeruhiwa vibaya mwaka wa 2021.

Hata hivyo Billie Eilish  ameibuka na kukanusha taarifa hizo kwa kusema kwamba hakuwa na nia ya kum-diss Travis Scott kama inavyotafsiriwa ila alikuwa anatoa msaada tu kwa shabiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *