Entertainment

Kanye West Aonyesha Furaha Baada ya Larry Hoover Kumpunguzia Kifungo, Atoa Shukrani kwa Drake

Kanye West Aonyesha Furaha Baada ya Larry Hoover Kumpunguzia Kifungo, Atoa Shukrani kwa Drake

Msanii maarufu wa Marekani, Ye (Kanye West), ameonyesha furaha yake baada ya Rais wa sasa wa Marekani, Donald Trump, kupunguza kifungo cha aliyekuwa kiongozi wa genge kutoka Chicago, Larry Hoover.

Ye alionyesha shukrani kwa msanii mwenzake Drake kwa mchango wake katika juhudi za kumkomboa Hoover, akitambua ushirikiano wao kama sehemu muhimu ya mafanikio haya.

“THANK YOU DRAKE FOR HELPING TO BRING LARRY HOOVER HOME.”, Aliandika X

Ye na Drake waliweka tofauti zao kando na kuungana kwa tamasha la pamoja mnamo mwaka 2021, likiwa ni sehemu ya kampeni ya kumtetea Hoover na kushinikiza kuachiliwa kwake. Tamasha hilo liliitwa Free Larry Hoover Benefit Concert na lilileta msukumo mkubwa kwa umma na viongozi kuhusu kesi ya Hoover.

Larry Hoover alikuwa akitumikia kifungo cha maisha kwa makosa ya uhalifu wa genge, lakini amekuwa akihusishwa na mabadiliko chanya akiwa gerezani. Uamuzi wa kupunguziwa kifungo wake umetajwa na baadhi ya watu kama hatua ya kihistoria katika juhudi za mageuzi ya mfumo wa haki nchini Marekani.

Kwa Ye, huu ni ushindi mkubwa kwa familia ya Hoover na kwa wale wanaoamini katika nafasi ya pili na msamaha wa kweli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *