Entertainment

Kanye West na Kim Kardashian wafikia muafaka wa Talaka yao

Kanye West na Kim Kardashian wafikia muafaka wa Talaka yao

Rapa Kanye West na Kim Kardashian hatimaye wamefikia maridhiano ya Talaka na sasa YE atatakiwa kumlipa Kim Kardashian kiasi cha ($200k) zaidi ya Sh. Milioni 22 kila mwezi kwa ajili ya matunzo ya watoto yaani Child support.

Kubwa zaidi lililofikiwa muafaka ni haki sawa katika malezi ya watoto (equal access) ambapo awali ilikuwa ngumu kwa YE kupata nafasi ya hata kuwaona watoto wake.

Japo imeelezwa kwamba watoto watatumia muda wao mwingi kwa Mama yao, jambo ambalo hata YE aliwahi kulipitisha.

Itakumbukwa, Mwanamama Kim Kardashian mwezi Februari, mwaka jana alifungua shauri mahakamani la kudai Talaka baada ya kuwa kwenye ndoa kwa takribani miaka 7 na Kanye West.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *