LifeStyle

Karole Kasita Asema Hana Mpango wa Kuolewa

Karole Kasita Asema Hana Mpango wa Kuolewa

Mwanamuziki wa Dancehall kutoka nchini Uganda, Karole Kasita, amefunguka kuwa hana mpango wa kuingia kwenye ndoa kwa sasa, akisisitiza kuwa nguvu zake zote kwa sasa amezielekeza kwa mtoto wake na kazi ya muziki.

Karole, ambaye alijifungua mtoto wake wa kwanza takribani miaka mitatu iliyopita, amefafanua kuwa ingawa hajaolewa na baba wa mtoto wake, lakini amemshukuru kwa kutimiza majukumu yake ya uzazi ipasavyo.

Amesema kuwa, ingawa watu wengine humuita mama asiye na mwenzi(Single Mother), anahisi si sahihi kwa sababu baba wa mtoto wake anashiriki kikamilifu katika malezi na matunzo. Ameongeza kuwa hana mpango wa kuolewa kwa sasa kwani anataka kujikita zaidi katika kazi na malezi ya mwanawe.

Msanii huyo anayefahamika kwa wimbo wake maarufu “Balance” amesema kuwa mtoto wake ndiye kipaumbele chake cha kwanza, na sasa hana muda wa kufikiria masuala ya mapenzi.

Karole Kasita anaendelea kung’ara kama mmoja wa wasanii wanawake wakubwa wa dancehall nchini Uganda, akijulikana kwa uimbaji wenye nguvu jukwaani na nyimbo zilizoteka anga la muziki wa Afrika Mashariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *