
Mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Uganda, Khalifah Aganaga amemtolea uvivu msanii Sheebah Karungi akimtaja kuwa na roho mbaya.
Aganaga anasema alishtuka baada ya Sheebah kushindwa kumualika kwenye tamasha lake katika Hoteli ya Serena jijini Kampala hivi karibuni licha ya kumkingia kifua alipokimbiwa na meneja wake, Jeff Kiwa.
“Ulikuja kwangu kipindi meneja wako alikukimbia, kila mtu alikuwa na shaka na uwezo wako kisanaa lakini nilikupa nyimbo, ukaweza kuteka nyoyo za mashabiki zako kwa mara nyingine. Lakini nimesikitishwa na kitendo cha wewe kunivunjia heshima,” alisema kwa uchungu.
Aganaga anasema kilichomuumiza zaidi ni kitendo cha Sheebah Karungi kuondoa nembo ya lebo yake ya Bad Character tabia kwenye wimbo wake wa “Bailamos.
Hata hivyo amesisitiza kuwa anataka kuthaminiwa wakati bado yupo hai na sio kufanyiwa figisu figisu kwenye shughuli zake za muziki.