
Rapa kutoka nchini Kenya Khaligraph Jones amefunguka sababu ya kutofanya kazi na wasanii wa nyimbo za injili.
Katika mahojiano na Mzazi Willy M. Tuza kwenye Mambo Mseto Khaligraph Jones amesema licha ya kuomba kufanya kazi ya pamoja na baadhi ya wasanii wa nyimbo za injili nchini wengi wao wamedinda kushirikiana naye kimuziki kwa hofu ya kukosolewa na mashabiki.
Khalighraph Jones ametoa kauli yake hiyo mara baada ya kuulizwa uhusiano wake na wasanii wa nyimbo za injili ukoje ikizingatiwa kuwa ana wimbo wa injili uitwao “Sifu Bwana” ambao amemshirikisha Nyashinski.