Entertainment

“Kifo cha PNB Rock kimenifanya niwe muoga”- Asema Lil Baby

“Kifo cha PNB Rock kimenifanya niwe muoga”- Asema Lil Baby

Rapa Lil Baby amefunguka na kusema kuwa baada ya kupata habari za kifo cha rapa mwenzake Pnb Rock kilichotokea Septemba 12 mwaka huu, amekuwa muoga hata wa kutoka nje.

Kupitia mahojiano aliyoyafanya na complex, Lil Baby amesema “Imekuwa kama simu ya kuniamsha, sio kwamba sijui kuna matukio kama hayo ila taarifa za kifo cha Pnb Rock zimenifanya niwe muoga hata wa kwenda kula kwenye migahawa mikubwa pia imenifanya niwe makini zaidi”

Utakumbuka Rapa PNB Rock aliuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia Septemba 12 kwenye tukio la uvamizi lililotokea kwenye mgahawa mmoja Jijini Los Angeles.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *