Gossip

KIM KARDASHIAN AKANUSHA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA KANYE WEST KUHUSU UWEPO WA SEXTAPE YAKE NA RAY J

KIM KARDASHIAN AKANUSHA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA KANYE WEST KUHUSU UWEPO WA SEXTAPE YAKE NA RAY J

Kanye West ameiambia Hollywood Unlocked kwamba alifanikiwa kuupata mkanda wa ngono kutoka kwa Ray J, ikiwa ni sehemu ya pili ya ule ambao ulivuja mwaka 2007 ukimuonesha Ray J na Kim Kardashian wakifanya mapenzi.

Kwenye mahojiano ambayo ameyafanya na Hollywood Unlocked, YE amesema Kim alitokwa na machozi baada ya kufikishiwa mkanda huo.

“Nilikwenda na kuchukua laptop mwenyewe kwa Ray J, na nilimpatia Kim Kardashian kwenye saa mbili asubuhi. Alilia sana baada ya kuona Laptop, unajua kwanini? Ni kwa sababu iliwakilisha namna gani watu walikuwa wanamtumia na kumchukulia kama bidhaa” alisema YE kwenye mahojiano hayo.

Wack 100 aliyekuwa meneja wa Ray J ndiye alitusanua uwepo wa sehemu ya pili ya mkanda huo wa ngono.

Masaa machache baada ya kutoka taarifa hiyo, upande wa Kim Kardashian umeibuka na kukanusha taarifa hiyo ikisema hakukuwa na maudhui yoyote ya ngono na hakuna sehemu ya pili ya mkanda huo.

Aidha kwenye laptop hiyo kulikutwa video za Kim na Ray J wakiwa kwenye ndege wakielekea nchini Mexico na zingine wakiwa kwenye kumbi za starehe na migawaha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *