Entertainment

King Saha aahirisha tamasha lake kutokana na matatizo ya kiafya

King Saha aahirisha tamasha lake kutokana na matatizo ya kiafya

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda King Saha ameripotiwa kuahirisha tamasha lake la muziki ambalo lilipaswa kufanyika siku ya wapendanao duniani, Februari 14 mwaka 2023.

Duru za kuaminika zidai kuwa mratibu wa tamasha hilo, Promota Musa Kavuma maarufu KT Promotions, pamoja na King Saha walianda mkutano wa faragha ambapo kwa kauli moja waliridhia kuahirisha tamasha hilo hadi pale itakapotangazwa tena.

“Haitatokea. Imeahirishwa,” msemaji wa KT Promotions, Eddie Ssendi alithibitisha.

Mabadiliko ya Tamasha la King Saha yamehusishwa na hali ya kiafya ya msaniii huyo ambaye alishauriwa na madaktari apumzike kabla ya kuanza tena shughuli zake za muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *