Entertainment

King Saha amshukuru Chameleone kwa kusimama naye wakati wa matatizo

King Saha amshukuru Chameleone kwa kusimama naye wakati wa matatizo

Mwanamuziki King Saha ni mwingi wa shukran kwa kitendo cha Jose Chameleone kutumbuiza kwenye shows zake alizokuwa ameratibu kutoa burudani kwa mashabiki zake.

King saha ambaye aliruhusiwa kuondoka katika hospitali ya Nakasero wiki iliyopita ambako alikuwa amelazwa, amefarijika na ukarimu waBosi huyo wa Leone Island kumkingia kifua alipokuwa kwenye matatizo ambapo amemtaja kuwa mtu mwema kuwahi kutokea nchini Uganda kwa upande wa wasanii.

“Namshukuru Chameleone kwa ukarimu wake. Namheshimu sana kwa kunifanyia shows zangu nilipokuwa nimelazwa hospitalini,” alisema.

King Saha kwa sasa amechukua mapumziko kwenye muziki wake kwa ajili ya kuiweka afya yake sawa kabla ya kuanza shughuli zake rasmi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *