Entertainment

KRG The Don Adokeza Kugombea Useneta Nairobi 2027 Kupitia Wimbo Mpya ‘Leo’

KRG The Don Adokeza Kugombea Useneta Nairobi 2027 Kupitia Wimbo Mpya ‘Leo’

Msanii wa muziki wa Kenya, KRG The Don, amedokeza uwezekano wa kuwania kiti cha useneta wa Kaunti ya Nairobi mwaka 2027 kupitia wimbo wake mpya uitwao “Leo.”

Katika video ya wimbo huo, mashabiki wamegundua bango linalosomeka “Hon. Stephen Kiruga Kimani – Senator Nairobi County. Vote!” jambo lililotafsiriwa kama ishara ya wazi kwamba msanii huyo ana mipango ya kuingia kwenye ulingo wa siasa.

Iwapo ataamua kuingia rasmi katika siasa, KRG The Don ataungana na orodha ya wasanii wa Kenya waliowahi kujaribu bahati yao kwenye uongozi wa kisiasa, akiwemo Jaguar, Bahati, na Prezzo.

Ikumbukwe kuwa awali KRG The Don alishawahi kutangaza hadharani nia ya kuingia kwenye siasa, ingawa hakutaja ni wadhifa upi atakaowania wala eneo gani atalisimamia kwenye uchaguzi ujao wa mwaka 2027.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *