Msanii wa muziki nchini KRG The Don amefufua tena bifu yake na wasanii wa sailors gang siku chache baada msanii wa kundi hilo Cocos Juma kudai kuwa lebo ya Black Market Records imesambaratisha muziki wao.
Kupitia ukurasa wake wa instagram KRG The Don amesema aliwaonya wasanii wa sailors gang kuhusu muziki wao lakini walimchukulia poa huku akienda mbali zaidi na kusema kwamba tamaa ya kutaka maisha ya haraka ndio imewaponza wasanii hao jambo ambalo analodai lilipelekea kuingia mkataba na lebo ya Black Market Records ambayo iliwapoteza kimuziki.
Bosi huyo wa Cash group Entertainment amedai masaibu yanayowaandama wasanii wa Sailors ni kutokana na kiburi waliowaonyesha wadau wa muziki nchini kipindi walipata umaarufu kubwa kwenye tasnia ya muziki nchini.
Hata hivyo amewataka wasanii wa Sailors Gang kuwaomba msamaha watu waliowadharau kipindi cha nyuma ili njia zao zianze kufunguka
Ikumbukwe KRG The Don na Sailors Gang waliachia wimbo wa pamoja uitwao “Nyandus” mwaka wa 2019 lakini lilopokuja suala la kutayarisha video walizozana kuhusiana na ishu ya malipo na hivyo ikasambaratisha mpango wa kuiachia video rasmi ya wimbo huo.