Entertainment

KRG THE DON ATANGAZA KUWASAJILI WASANII WAPYA KWENYE LEBO YAKE YA FAST CASH GROUP MUSIC

KRG THE DON ATANGAZA KUWASAJILI WASANII WAPYA KWENYE LEBO YAKE YA FAST CASH GROUP MUSIC

Msanii wa muziki wa dancehall nchini KRG The Don ametangaza mpango wa kuwasajili wasanii wapya kwenye lebo ya muziki ya Fast Cash Group music.

Kupitia ukurasa wake wa instagram KRG The Don amewataka mashabiki zake wamuunganishe na wasanii wenye vipaji kwenye muziki kwani lebo ya fast cash Group ipo tayari kuwasaidia kimuziki.

Hata hivyo amewataka mashabiki na wasanii chipukizi waendelee kufuatilia mitandao ya kijamii ya Fast Cash Group kwa lebo hiyo itatoa tamko rasmi hivi karibuni ya kufanikisha mchakato mzima wa kuwasajili wasanii.

“Lebo ya muziki ya Fast Cash Group ina habari njema kwa wasanii wachanga wenye vipaji kama unamjua msanii ambaye ana kipaji mwaambie kwamba lebo ya Fast Cash Group ipo tayari kumsaidia kimuziki ila kwa sasa endeleeni kufuatilia Fast Cash Group music kupitia mitandao yetu ya kijamii mwaka huu tuna mazuri kwa ajili yenu” amesema KRG The Don kupitia Instagram page yake.

Utakumbuka lebo ya muziki ya Fast Cash Group ambayo makao yake makuu yapo South B jijini Nairobi ilizinduliwa miaka saba iliyopita na  KRG The Don  kwa ajili ya kurekodi kazi za wasanii na muziki wake mwenyewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *