Entertainment

Lava Lava Apata Ubalozi Wake wa Kwanza Tangu Kuondoka WCB

Lava Lava Apata Ubalozi Wake wa Kwanza Tangu Kuondoka WCB

Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Lava Lava, ametangaza rasmi mkataba wake wa kwanza wa ubalozi tangu alipoondoka kwenye lebo ya WCB Wasafi. Msanii huyo sasa ni balozi wa kampuni ya kuuza magari ya Khushi Motors Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi rasmi wa yard ya kampuni hiyo, Lava Lava alisema amefurahia kushirikiana na Khushi Motors, ambayo inalenga kuwasaidia Watanzania wengi kupata magari kwa bei nafuu na zinazolingana na hali ya maisha ya watu wa kawaida.

“Khushi Motors ipo kwa ajili ya kuhakikisha kila Mtanzania anapata gari analolitamani kwa bei inayomuwezesha,” alisema Lava Lava wakati wa tukio hilo, huku akionyesha furaha yake kwa hatua hiyo mpya kwenye maisha yake ya sanaa na biashara.

Ubalozi huu unakuja kama ishara ya mwanzo mpya kwa Lava Lava baada ya kujitegemea nje ya WCB, na mashabiki wake wengi wamepongeza hatua hiyo, wakimtakia mafanikio zaidi ndani na nje ya muziki.

Kwa sasa, Lava Lava anatarajiwa kushiriki katika kampeni mbalimbali za masoko za Khushi Motors, ikiwa ni pamoja na matukio ya mauzo, promosheni na kampeni za kidigitali kupitia mitandao ya kijamii.