Entertainment

Maandy azima tetesi za kutoka kimapenzi na Breeder LW

Maandy azima tetesi za kutoka kimapenzi na Breeder LW

Rapa Maandy kwa mara nyingine amekanusha madai yote kwamba yeye na msanii Breeder LW ni wapenzi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwajibu mashabiki zake waliokuwa wakidhani kwamba wanachumbiana, Maandy amethibitisha kwamba madai hayo hayana ukweli wowote.

Hitmaker huyo wa ‘Ni Wetu’ ameeleza kwa kina kwamba mwanamke aliyepiga picha na Breeder LW wakiwa kwenye mahaba mazito, siku moja baada ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake sio yeye.

Maandy amedai kwamba alipata taarifa ya kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na rapa huyo kupitia simu za marafiki zake, huku akiwataka mashabiki kuacha tabia ya kumhusisha kimapenzi na Breeder LW ikizingatiwa kuwa hakuna kitu kinaendelea kati yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *