
Mwanamuziki na mfanyabiashara maarufu wa Marekani, Sean “Diddy” Combs, amepatikana na hatia ya kosa la ukahaba haramu lakini amesafishwa mashtaka mazito zaidi ya biashara haramu ya ngono (sex-trafficking) na uhalifu wa kupanga (racketeering), ambayo yangemuweka gerezani maisha.
Kufuatia hukumu hiyo, mchakato wa kutoa adhabu rasmi umekamilika na sasa unatarajiwa kutangazwa rasmi hivi karibuni. Diddy anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 20 jela kwa kosa hilo la ukahaba haramu. Wanasheria wake wameshikilia kuwa anapaswa kuachiliwa kwa dhamana akisubiri kusikilizwa kwa hukumu yake rasmi, wakisisitiza kuwa hana historia ya kukimbia kesi.
Hata hivyo, upande wa mashtaka unapinga vikali ombi hilo, ukionya kuwa Diddy ana ushawishi mkubwa wa kifedha na kijamii unaoweza kutumiwa kuingilia mchakato wa haki.
Kesi hii imeibua mjadala mkubwa duniani kuhusu matumizi mabaya ya mamlaka, ushawishi wa mastaa katika vyombo vya sheria, na mapambano dhidi ya unyanyasaji wa kingono.