
Msanii wa Bongofleva, Malkia Kareen amesema mwaka huu asiposhinda tuzo kupitia wimbo wake mpya, Te Quiero ataacha muziki.
Malkia Kareen amesema hayo kupitia XXL ya Clouds FM ambapo ameeleza wimbo huo anauona ukienda kufanya vizuri kwenye tasnia ya muziki Afrika Mashariki.
“Nikikosa tuzo mwaka huu na huu wimbo naachana muziki,” amesema Malkia Karen.
Utakumbuka Aprili mwaka 2021 Malkia Karen alifanikiwa kushinda tuzo mbili za Zikomo Awards kutoka nchini Zambia katika vipengele vya Best Female Artist Africa na Best Song of the Year kupitia wimbo wake, Sina.